Taarifa kuhusu dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyosambazwa na MSD

Bohari ya Dawa, ni Idara  chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 13 ya mwaka 1993.  Majukumu yake  ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa, vifaa tiba, vitendanishi na chanjo katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali, mashirika ya dini na yasiyo ya kiserikali . Aidha, Bohari ya Dawa inahusika katika usambazaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya misaada chini ya miradi misonge (vertical programmes) ya kupambana na malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu.

Usambazaji katika mwaka 2010/11:
Kwa kipindi cha Julai 2010 hadi Juni 2011, Bohari ya Dawa ilisambaza dawa, vifaa, vifaa tiba, vitendanishi na chanjo zenye thamani ya Tsh Bilioni 134.  Kiwango hicho kinahusisha dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa na kuuzwa na Bohari ya Dawa kinachofikia Tshs Bilioni 55.8. Aidha, ilisambaza  dawa, vifaa, vifaa tiba, vitendanishi na chanjo za misaada chini ya  miradi msonge vya thamani ya ni Tsh 78.3

Ripoti hii inatolewa kama taarifa rejea kwa wadau wote na wananchi kwa ujumla ili waweze kujua ni kiasi gani cha dawa na vifaa tiba vimesambazwa na Serikali wategemee huduma gani kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.

Bofya hapa chini ili kushusha taarifa hii.

Tags: 
AttachmentSize
Taarifa kwa umma.pdf487.46 KB

News & Events